Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mushizo Afunguka A – Z Ajali ya Moto, Aamini Uchawi

Msanii wa singeli na Dj maarufu nchini, Mushizo ameeleza tukio la ajali ya moto iliyomtokea nyumbani kwake Tabata, Juni 12, 2025, ni mipango ya Mungu na si vingenevyo.

"Mimi naamini ni mipango ya Mungu kwa sababu hayo matatizo yanatokea kila siku na ikitokea ni mara chache sana mtu kupona. Kwahiyo kwangu mimi ni mipango ya Mungu, sio ajali ya kitoto pale nilipokuwepo moto ulipotokea hakikubaki kitu chochote. Na hata mimi mwenyewe nilishindwa kujiokoa nilizimia nikastuka nipo hospitali," amesema Mushizo.

Mushizo ameongezea kuwa hata yeye haelewi chanzo cha moto huo kwani ajali hiyo ilimtokea akiwa amepumzika ndani baada ya mchoko.

"Nakumbuka nilikuwa kwenye shoo Mwanza kama wiki nzima, nilivyorudi jioni nikataka kupumzika, ile kupumzika mpaka inafika saa moja kasoro ndio hilo tukio likatokea," amesema Mushizo.

Hata hivyo DJ huyo amesema changamoto aliyopitia haijamvunja moyo bali imemuongezea nguvu ya kuendelea kufanya kazi zaidi.

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: