Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bahati Apima DNA na Mwanamke Anaedaiwa ni Mama Yake

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Bahati hatimaye amekutana na mwanamke anayedaiwa kuwa ni Mama yake Judith Makokha na kuchukua hatua ya kwenda kupima naye vinasaba (DNA).

Mwisho wa mwaka 2025, mwanamuziki huyo alizungumzia suala hilo baada ya mwanamke huyo kusambaa kwenye mtandao ya kijamii akidai kuwa yeye ndiye Mama yake Bahati.

Judith alitoa video iliyosambaa akimuomba Bahati msamaha kwa madai ya kumtelekeza zamani. Aliongeza kuwa miaka mingi iliyopita hakuwa na uwezo wa kifedha wa kumtunza mwanawe, na kwamba alilazimika kumwacha katika kituo cha watoto yatima.

Bahati alivutiwa na simulizi ya Judith lakini alisisitiza kuwa aliwahi kushuhudia mazishi ya Mama yake mzazi miaka iliyopita.

Bahati alikuwa na mashaka kwa sababu alikulia akijua anatoka kabila la Wakamba ilhali mwanamke huyo ni Mluhya.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: