Ikiwa imepita Zaidi ya miaka 20 tangu wimbo ambao haushi radha vizazi na vizazi wa ‘Nimekuchagua wewe’ kutoka kwa Bob Rudala na sasa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Phina ameamua kuurudia tena wimbo huo huku akiwa na mpenzi wake kutoka Nigeria, Eni.
Phina ameshare kionjo cha wimbo huo kupitia ukurasa wake wa instagram wimbo ambao unatarajiwa kutoka rasmi Jumapili hii, Novemba 16.
Mbali na wimbo huo Phina, akiwa pamoja na mpenzi wake Enioluwa, wamerikodi nyimbo mbalimbali ikiwemo “Mungu Ibariki Tanzania” na “Smile For Me” ya Simi.
Chanzo; Mwananchi Scoop