Mfanyabiashara na mwanamuziki P Diddy ametupwa jela miaka 4 na miezi miwili baada ya kukutwa na hatia mbili ikiwemo ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya shughuli za ukahaba.
Hukumu hiyo imetoka ikiwa ni miezi mitatu tangu msanii huyo akutwe na hatia.
Awali, masaa kadhaa kabla ya hukumu yake Oktoba 3,2025, P Diddy alituma barua ya msamaha kwa Jaji wa kesi yake akimuomba msamaha Cassie dhidi ya kitendo alichomfanyia.
Zaidi, Timu yake ilitoa video za msanii huyo akiwa na wanawe za kabla na baada ya P Diddy kuwekwa jela zenye kumtia neno la faraja dhidi ya matukio yote aliyokuwa nayo Diddy hadi kusweka jela miaka 4 na miezi miwili.
Chanzo: Tanzania Journal