Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mtoto wa Ronaldo Aliyetema Mpira na Kuibukia Udj

Katika maisha ya ndoa ya mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldo De Lima tunagusia mmoja wa watoto wake wa kiume ambaye ameamua kuachana na masuala ya soka na kuwa DJ wa muziki. Twende pamoja!

Kati ya watoto wanne wa Ronaldo de Lima (49), ni mmoja tu, Ronald (25) ndiye alionyesha nia ya kufuata nyayo za baba yake katika soka, lakini baadaye akaamua kuwa DJ, kazi anayoifanya hadi sasa.

Katika hili unaweza kusema Ronaldo ni kama kasalitiwa na wanawe,kwani watoto wake wengine watatu wamechagua kufanya vitu vingine nje ya soka. Kwa leo, tutamtazama kiundani Ronald ambaye ni mtoto wa kwanza wa Ronaldo aliyempata katika ndoa yake ya kwanza na mwanasoka, Milene Domingues ambaye ndoa yao ilidumu kwa miaka minne.

Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid, akiwa katika kilele cha mafanikio yake, mnamo 1999, alifunga ndoa na Milene ambaye kwa sasa ni mchambuzi maarufu wa michezo nchini Brazil.

Kufikia Aprili 6, 2000, huko Milan nchini Italia, wakajaliwa mtoto wao wa kwanza waliyempa jina la Ronald ambalo linatofautiana kidogo sana na la baba yake mzazi. Mama yake Ronald, Milene, pia alikuwa mchezaji akiichezea timu ya taifa ya Brazil mara 20 na kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kupiga danadana zaidi ya 55,000 bila kuangusha mpira akiwa na umri wa miaka 17.

Kuwa na wazazi wenye vipaji hivyo, wengi walidhani Ronald angekuja kuwa mchezaji mkubwa wa soka duniani na kuweka rekodi mbalimbali kama wazazi wake lakini haikuwa hivyo. Badala yake, Ronald aliamua kuwa DJ, akitumia jina lake kama utambulisho wake. Inasemekana baba yake, ambaye ni mpenzi mkubwa wa muziki, alimtia moyo pindi alipochagua kazi hiyo.

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: