Baada ya miaka minne kupita kesi ya mauaji ya msanii kutoka kundi la Migos marehemu TakOff imepangwa kuanza kusikilizwa novemba 5 mwaka huu 2026.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo anayefahamika kwa jina la PatrickClark alihudhuria kikao cha awali cha kesi (pre trial hearing) katika Mahakama ya Kaunti ya Harris, Wakati wa kikao hicho, tarehe ya kuanza kwa kesi ilipangwa kuwa Novemba 5.
Msanii TakeOff alifariki kwa kupigwa risasi na kufariki hapo hapo (Novemba 1 2022) baada ya kutokea mzozo uliyosababishwa na kupishana kauli kwa watu waliokuwa wakicheza kamari hali iliyopelekea kufyatuliana risasi na kuchukua uhai wa msanii huyo.
Chanzo; Eatv