Mtoto wa Wizkid, wa kwanza Champz jina halisi Boluwatife Balogun, aanza kuziweka rekodi mithili ya Baba yake akiwa bado kijana mdogo miaka 14, ameshika nafasi ya kwanza Spotyfy Nigeria na 71 United Kingdom “Uk” na kumpa wadhifa wa kuwa kijana mwenye umri mdogo kutundika rekodi hiyo nchini kwao.
Ameiweka rekodi hiyo mara baada ya kuachia Ep yake Novemba 11,2025 ya “Champion Arrival” ambayo ameenda kama karapa wa kizazi kipya, akikiwakirisha kizazi cha vijana wenye umri mdogo kwenye muziki Nigeria na njee ya viunga vyake.
Licha ya kuzaliwa kwenye familia ambayo tayari ana ustaa kisa mshua wake lakini yeye binafsi ameanza kuzitembea hatua za umaarufu wake kwenye muziki wake wa rap kama mshua wake.
Chanzo; Tanzania Journal