sanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ibraah amelia na Mashekh nchini akitaka ufafanuzi iwapo mwanamke wa kiislam anaweza kumuacha mumewake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah amewatag baadhi ya mashekh nchini na kuandika; "FAMILY ❤️ RAMADHANI KAREEM ☪️💜Naomba muwatag mashekhe ambao nita wasahau kwenye hii post. Maana ninahisi funga yangu ita tetereka wanisaidie hili.
"Hivi katika Uisilam inaruhusiwa mwanamke kumuacha mwanaume au ni mwanaume kumuacha mwanamke tu maana nimeachwa na ninaye muita mke wangu" ameandika Ibraah.
Chanzo; Mwananchi Scoop