Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mama Amina Atua kwa Chino Wanaman

Huenda mwimbaji nyota wa Bongofleva toka Wanaman Gang, msanii Chino Kid, ameendelea kupanua wigo wake katika tasnia ya muziki baada ya kumkaribisha msanii wa Singeli, Mama Amina, kwenye lebo yake ya Wanaman Gang.

Chino ambaye anafanya vizuri kwasasa kupitia ngoma iitwayo Mlegezo, maswali yamekuwa mengi kwa mashabiki kupitia post yake ya leo Jumapili, wakihoji je mkali huyo ame-msanii Mama Amina Wanaman Gang?

"Karibu Wanaman Gang Mama Amina, hili ndio chama la wana kutoka mitaani,"  Ameandika Chino Kid kupitia ukurasa wake.

Aidha, jambo hili ambalo bado halijathibitishwa na pande zote mbili, lakini kwa upande mwingine Mama Amina kufanya kazi chini ya lebo ya Wanaman Gang kutampa usimamizi wa kitaalamu na mazingira bora ya kisanii.

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: