Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bad Bunny Mtoto wa Dereva na Muuza Duka, Kabla ya Ustaa

Benito Antonio Martínez Ocasio, ndilo jina halisi la Bad Bunny. Moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa kizazi hiki. Alizaliwa Machi 10, 1994, huko Bayamón, Puerto Rico na kukulia kijiji cha Vega Baja. Akilelewa katika familia ya tabaka la kati. Baba yake alikuwa dereva wa lori na mama yake mkufunzi wa Kiingereza.

Bad Bunny alianza kuimba akiwa mdogo, akijifunza muziki kanisani kabla hata hajafikisha miaka 13. Alianza kuunda midundo yake mwenyewe na kuandika mistari ya muziki akiwa shuleni, huku akitumia muda wake wa ziada kujifunza zaidi kuhusu muziki.

Jina lake la sanaa 'Bad Bunny' lilitokana na picha yake ya utotoni akiwa amevaa koti la sungura. Picha ambayo ilamfanya aitumie kwenye kupata jina kwani aliamini kwenye biashara itakuwa rahisi watu kukumbuka kirahisi.

Alisomea katika Chuo Kikuu cha Puerto Rico, Arecibo. Lakini wakati huohuo alianza kupakia nyimbo zake kwenye SoundCloud mwaka 2013. Ilipofika mwaka 2016, wimbo wake 'Diles' ulimvutia mtayarishaji wa muziki maarufu DJ Luian na kumpa mkataba wake wa kwanza wa kurekodi, jambo lililomuwezesha kuingia rasmi kwenye tasnia ya muziki.

Bad Bunny aliwahi kufanya kazi katika duka la vyakula (supermarket) linaloitwa Econo huko Puerto Rico kabla hajapata umaarufu mkubwa kwenye muziki. Wakati huo alikuwa bado anasoma katika chuo. Dukani hapo alikuwa akifanya kazi kama mpangaji na mfungaji wa bidhaa dukani hapo.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: