Rapa @nelly anasema kizazi chake alichotoka nacho kwenye muziki kilikuwa kizazi kigumu zaidi kwenye historia ya muziki wa HipHop.
Nelly anasema alikuja katika kipindi chenye ushindani mkubwa ambao wasanii wengi wakali walikuwa wanataka kuwa namba 1 mwanzoni mwa miaka ya 2000.
đź—Ł"Kizazi changu kwenye muziki kilikuwa kizazi kigumu kwenye historia ya muziki wa HipHop".
"Kila nikitoa wimbo kulikuwa na wasanii kama DMX, Jay Z, Eminem,50 Cent,Lil Wayne, Ludacris. Wote hao walikuwa wanapambana namba 1" amesema Nelly
Nelly ameongeza kusema wakali wote hao walitawala kwa njia tofauti, walirap tofauti, kutoa style mpya na ushindani wa hali ya juu.
Chanzo; Eatv