Nimekuwa ni msanii ambaye nimepata mafanikio makubwa sana kuliko wasanii wote wa sasa. Wasanii wa sasa Wana mafanikio makubwa kunizidi kwa muda wangu Mimi hakuna aliyekuwa akinifuata labda niweke heshima kwa Lucas Mkenda, Mr Nice. Baada ya kutoka Mr Nice nikaingia Mimi. Nilipata mafanikio makubwa sana.
" Nilikuwa nimetoka mtaani tu , Ilala. Niliona washkaji na marafiki ndio kila kitu. Nilikuwa natembea na watu wengi sana. Joseph Kusaga aliwahi kuniita kwenye gari akiwa na Koffi Olomide, Leaders Club akaniambia natembea na watu wengi sana. Nawezaje?”
"Pia hata Ruge Mutahaba aliwahi kuniambia hivyo. Yeye aliniambia ataniadhimu hapendezwi ninavyoishi. Kutoka kule na huwambiwi na mtu usifanye jambo fulani na una pesa nyingi unakutana na vitu ambavyo hujui ulikutana navyo wapi! Hata sijui dawa za kulevya nimekutana nayo wapi.” - Chidi Benz
Stori hii inapatikana kwenye ukurasa wa instagram wa Cloudstv.