Wakati jamii na wadau wa muziki ikiitambua WCB yani Wasafi Kama Lebo ya Muziki maarufu toka Tanzania inayomilikiwa na msanii maarufu Diamond Platnumz, moja ya mameneja wa msanii huyo Sallam Sk, adai kutoitambua lebo hiyo kama lebo bali anaitambua kama Shirika lisilo la kiserikali lililoamua kusaidia wanamuziki.
Meneja huyo aliyefanikisha kwa kubwa kuusafirisha muziki wa CEO wa lebo hiyo njee ya Mipaka ya Tanzania na Afrika kiujumla, ameweka wazi hayo kwenye Podcast ya Dozen Selection inayoendeshwa na Mtangazaji maarufu nchini Hamis Mandi wengi humwita Bdozen huku akidai haijawahi kuingiza faida yoyote tangu ianzishwe.
“Mimi siiti music lebo naweza kuita NGO ya kusaidia wanamuziki. Muwekezaji kabisa ni Diamond, percent zinazogawanywa haziko favour kwenye lebo ziko kwa wasanii. Naiita WCB NGo” - Sallam Sk
Pia meneja huyo akaeda mbali kwa kusema WCB haijwahi kupata faida kulingana nauwekezaji waliowekeza kwa wasanii kuhakikisha majina yao yanasimama na wengine kutaka kutoka mara baada ya majina yao kuwa makubwa.
Ikumbukwe, WCB, kwa Tanzania ni moja lebo licha ya meneja kutotambua hivyo bali imekuwa ikitambulishwa hivyo hata kwenye majukwaa yao ya kidijitali, ambayo imefanikisha kutambulisha vichwa vikubwa vya muziki nchini akiwemo Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Dvoice pia msanii Rich Mavoko amewahi pita kwenye lebo hiyo.
Chanzo: Tanzania Journal