Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Nizhny Novgorod Ilivyozizima Ufunguzi wa World Youth Festival Assembly

Usiku wa alhamisi Septemba 18 uliligeuza jiji la Niznhy Novgorod kuwa kitovu cha burudani nchini Urusi ikiwa ni katika ufunguzi wa Kongamano la Dunia na Kusanyiko la Vijana.

Burudani hiyo ambayo ilikuwa sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya kusanyiko kubwa la vijana toka mataifa mbalimbali duniani ilishuhudiwa na watu takribani 2000 ambao kwa pamoja macho yalikuwa stejini kujionea historia, mila na utamaduni wa Urusi vikionyeshwa.

Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Makamu Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Chernyshenko alieongozana na Grigory Gurov, Mkuu wa Wakala wa Masuala ya Vijana (Rosmolodezh). 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Waziri Mkuu aliwaeleza vijana lengo la nchi Urusi kuwa kitovu cha vijana kukutana na kuhakikisha ndoto na matarajio yao yanakuwa kweli kupitia ushirikiano baina yao. Aliongeza kusema kwamba Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin ana matamanio ya kuona vijana wanakuwa chachu ya kuleta mabadiliko duniani.

“Ni muhimu kuona majadiliano yanaendelea. Malengo ya kongamano yataendelezwa na klabu za kila nchi zilizoanzishwa ili kuleta mabadiliko chanya na kukuza fursa za majadiliano baina ya vijana na wanawake waliokuja Urusi kutoka mataifa mbalimbali. Nawatakia kila la heri katika kutimiza malengo haya”, ulisema ujumbe wa Rais Putin.

Kilele cha ufunguzi huo kilishuhudia burudani mbalimbali zilizounganishwa na historia ya nchi ya Urusi zikitolewa zikionyesha yaliyojiri toka karne zilizopita mpaka sasa, huku wasanii mbalimbali maarufu wakipanda jukwaani kutoa burudani kwa vijana hao.

Kongamano la Vijana Duniani linaandaliwa na Shirikisho la Masuala ya Vijana (Rosmolodezh), kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Niznhy Novgorod limeendelea kwa siku ya tatu likiwakutanisha vijana 2000 toka mataifa mbalimbali likilenga kufungua ushirikiano baina ya vijana duniani kote ambapo mada mbalimbali kuhusu ujasiriamali, ubunifu, vyombo vya habari na masuala ya kijamii vimeendelea kuwa sehemu kubwa ya mjadala.

Kuhusiana na mada hii: