Kimbembe Roma Vs Joh Makini, Kila Mtu Anavutia Kwake
kusema Roma Mkatoriki anarap flow moja akijibu swali aliloulizwa, Roma ameibuka kupitia kiwanja chake cha Instagram na kujibu aliyoyasema Joh Makini.
"I thought tumekua watu wazima sasa, Ivan anaingia form 1, King ana miaka 10 now! Naona umeshindwa ku-move on? Come on…. move on chalii!. Unataka turudi tulipotoka? I am ready! Though now nime-focus sana na mambo ya siasa na kuwasemea wananchi wetu.usinitoe kwenye reli!," ameandika Roma.
Hata hivyo Roma ameendelea kuandika kuwa kubadili floo kwa Joh Makini ndio kumempoteza na mpaka sasa watu hawampi sikio kwenye muziki wake.
"Huko unakokuita wewe kubadili kwako flow ndio kunazidi kukupoteza kwenye mchezo homies wako hawakuchani ukweli!. Nobody is paying attention to your music now. Wimbo wako wa mwisho kufanya vizuri (angalau) ni MCHELE (6Years Ago). That means una miaka 6 hujaweka chuma, ingawa umetoa utitiri wa nyimbo kama 24 hivi flow hazijasaidia kitu hata shows zako bado una-perfom old songs na sio hizi mpya coz no one knows them.
"Go back to your roots mangi! Ile radio ilikusaidia sana those days huo ndio ukweli, Mambo yalivyochange nyama imekuwa ngumu apart from that, you are a good rapper na inspiration kwa rappers wengi. Naheshimu art yako! You are a family man too, hii naipenda zaidi kutoka kwako! Next time kuwa makini na majibu unapoulizwa swali kuhusu watu. Au fanya tafiti kwanza," - Roma Mkatoriki
Zaidi, Joh Makini, kwenye interview na East Afrika Radio alisema yeye na Nikki wa Pili ni watu wazito kwenye kiwanda cha muziki na wala sio wao waliomkimbia backstage kama Roma, ambavyo amewahi kudai kwenye moja ya mistari yake.
Chanzo: Tanzania Journal