Wakitajwa waigizaji 10 bora kutoka India jina la Hrithik Roshan nyota anayefanya vizuri katika filamu za Bollywood lazima liwepo.
Licha ya mafanikio yake ipo simulizi ya maumivu, kejeli na masimango aliyokumbana nayo tangu akiwa mdogo. Hrithik Roshan ambaye alizaliwa mwaka 1974 akiwa na hali ya kimaumbile inayojulikana kitaalamu kama ‘Polydactyly’ yaani kuwa na kidole cha ziada, kwenye mkono wake wa kulia.
Kwenye mahojiano yake mbalimbali aliyowahi kuyafanya alisema akiwa shuleni alikumbana na udhalilishaji, kudhihakiwa na wanafunzi wenzake wakimcheka huku baadhi wakiogopa kukaa naye.
Aidha kwa muda mrefu, Hrithik alijifunza kuuficha mkono wake wa kulia ili wanafunzi wenzake wasione kidole cha ziada. Hata hivyo, changamoto zake hazikuishia hapo, mbali na hali ya vidole sita, alikumbwa na tatizo la kigugumizi (stammering) lililomtesa tangu utotoni.
“Nilikuwa mtoto asiyejiamini kabisa. Watoto waliniona tofauti, na hilo liliniumiza sana. Nilikuwa na kigugumizi kibaya sana. Kulikuwa na nyakati niliogopa hata kusema neno moja darasani,”
Chanzo; Mwananchi Scoop