Mshereshaji maarufu nchini na Mchekeshaji MC Pilipili amefariki Dunia mchana wa leo katika Hospitali jijini Dodoma.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Pilipili aliumwa ghafla mchana wa leo, ndugu wa karibu walimkimbiza hospitalini ambako muda mfupi baadae umauti ulimfika.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu tutazileta punde baada ya tamko la familia! Pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki ambao wameondokewa na mpendwa wao.
Chanzo; Clouds Media