Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Msanii Davido na Milango ya Ubunifu wa Mavazi Tanzania

Wabunifu wa mavazi nchini Tanzania, Kelly Evara pamoja na Muonekano, wameeleza kuwa wamepata mafanikio makubwa tangu walipopata nafasi ya kumvalisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido.

Wakizungumza kuhusu hatua hiyo, wabunifu hao wamesema kazi hiyo imewapa mwanga mkubwa kimataifa, huku wakieleza kuwa sasa wanafahamika zaidi nje ya mipaka ya Tanzania na kupokea mawasiliano mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa mitindo barani Afrika na kwingineko.

Muonekano ameongeza kuwa mbali na umaarufu, wamefanikiwa pia kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kupitia kazi hiyo, japokuwa hakutaka kuweka wazi kiwango halisi cha mapato waliyoyapata. Ameeleza kuwa tukio hilo limewapa motisha kubwa ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuinua hadhi ya mitindo ya Tanzania kwenye ramani ya dunia.

Kwa upande wao, wabunifu hao wamesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushahidi kuwa vipaji vya ndani vina uwezo wa kushindana kimataifa endapo vitapata fursa na sapoti stahiki.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: