Carmen Andrade, mmoja kati ya pacha walioungana mwenye umri wa miaka 25, amefunga ndoa kimyakimya na mpenzi wake wa muda mrefu, Daniel McCormack, katika harusi ya faragha iliyofanyika mwezi Oktoba huko Connecticut, baada ya kukutana mwaka 2020.
Wanandoa hao raia wa Marekani, walitangaza habari hiyo kupitia video ya YouTube, wakieleza kuwa ni Carmen pekee ndiye aliyeolewa, huku dada yake Lupita akiendelea kuwa 'single' na akijitambulisha kama mtu asiyevutiwa na masuala ya mapenzi.
Lupita amesema hana nia ya kuolewa, na dada hao wanaendelea kuishi pamoja kwa kuheshimiana na kuelewana.
Chanzo; Global Publishers