Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Master J Sababu za Kuchukiwa na Kutozungumza na Baba Yake

anasema maisha ni kuchagua na hivyo ndivyo alivyofanya mzalishaji wa muziki mkongwe nchini na mwanzilishi wa MJ Production ‘MJ Records’, Joachim Marunda ‘Master J’ ambaye licha ya kupata Shahada ya Uhandisi wa Umeme chuo kikuu cha London aliamua kuweka kabatini vyeti vyake na kuutumikia muziki.

Master J ambaye alianza uzalishaji muziki mwaka 1996 baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu amesema kitendo cha kuweka vyeti kabatini kilifanya asizungumze na baba yake kwa zaidi ya miaka minne.

“Mzee hakufurahi hatukuongea kama miaka minne, mitano. Ilifika muda akanifukuza nyumbani haikuwa suala la kufurahia. Hakukuwa na biashara ya muziki, kwanza hata redio hazikuwapo,” anasema.

Hata hivyo kumekuwa na tabia kwa baadhi ya vijana wa kileo ‘Gen Z’ kumshushia maneno ya lawama, kejeli na matusi mkongwe huyo kila anapojaribu kutoa mitazamo yake kuhusu muziki. Akizungumzia hilo anasema sababu kuu ya watu kumpinga ni chuki.

“Watu wana chuki na mimi kwa sababu nasema ukweli kuhusu wasanii wao. Hawapendi naongelea mpaka mapungufu lakini mimi siyo kama nachukia, naongea ili tuboreshe. Kwa hiyo kila msanii ambaye nitamuongelea kwenye mapungufu wanachukia na kutukana.

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: