Mkali wa Amapiano anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki Toss ameibua mjadala mzito katika mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kuwa kwenye mahusiano na aliyekuwa mpenzi wa Marehemu AKA, Nadia Nakai.
Mijadala hiyo imekuja baada ya Toss kuposti picha akiwa na Nadia akimtakia kheri katika Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), picha hizo ziliwaonesha wawili hao wakiwa katika sehemu ya ufukwe huku wakiwa katika penzi zito.
Katika chapisho lake, Toss aliweka nukuu ya Biblia inayosomeka “1 Wakorintho 13:4–8 type of love,” nukuu hiyo ikiwa na maana ‘Upendo wenye subira na wema’, huku Nakai akikomenti ujumbe mfupi “Happy Valentine’s Day!” bila maelezo zaidi.
Machapisho hayo yameibua maoni tofauti, ambapo baadhi ya mashabiki wameeleza huenda wawili hao wanatambulisha uhusiano wao mpya, wakati wengine wakieleza maisha binafsi ya Nakia kuwa ameamua kuendelea na maisha mengine baada ya kifo aliyekuwa mpenzi wake, rapa AKA, aliyeuawa kwa kupigwa risasi jijini Durban Februari 2023.
Aidha Toss hakuishia hapo alihamia tena Instagram Stories akishare video akiwa ametembelea banda la biashara ya urembo ya Nakai lililopo ndani ya Mall of Africa, ambako msanii huyo hivi karibuni alizindua chapa yake ya vipodozi iitwayo Naked Without by Bragga Cosmetics.
Hata hivyo hadi kufikia sasa wawili hao hawajatoa kauli rasmi kuhusu ukaribu wao, jambo ambalo linaloendelea kuwaacha mashabiki njia panda.
Chanzo; Mwananchi Scoop