Msanii Diamond Platnumz, anatarajiwa kuandika historia Mpya nchini Sierra Leone tarehe 19 Desemba 2025, ambapo atatumbuiza live katika Chapter One, VIP iliyopo Jijini Freetown.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, kiingilio cha V.I.P ni $5k (Tsh. Milioni 12.2/=), huku V.i.p ya kati ikiwa ni $1k (Tsh. Milioni 2.4/=) na kwa kawaida ikiwa na gharama ya $100, sawa na takribani shilingi 245,000 za Kitanzania.
Hii inaendelea kuonesha jinsi thamani na hadhi ya Diamond Platnumz zinavyozidi kukua kimataifa, akibaki kuwa miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaotoza viwango vya juu zaidi katika shows zake za muziki.
Chanzo; Wasafi