Mwanamuziki wa Nigeria, Asake ameripotiwa kumaliza na tofauti na babayake mzazi, mzee Odunsi Fatai baada ya kuwa na migogoro ya kifamilia kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa katika mitandao ya kijamii staa huyo alimaliza tofauti na baba yake mwishoni mwa Desemba 2025, ambapo alikutana tena na baba yake na kumzawadia nyumba pamoja na kumlipia bili za hospitali. Hatahivyo imeelezwa kuwa hali ya amani kati ya Asake na familia yake imerejea tena baada ya kutoelewana kwa muda wa miaka mitatu.
Tukio hilo limetafsiriwa kama ishara nzuri kwa familia ya Asake, huku mashabiki wakimpongeza Mr. Money kwa kurudisha huduma na mawasiliano mazuri kwa familia yake.
Asake na familia yake inaelezwa walikutana sikuchache kabla ya sikukuu ya Chrismass ya mwaka 2025, huku familia hiyo ikionekana kuwa na tabasamu na ishara ya upendo, kuashiria kuisha kwa mivutano ya zamani katika familia hiyo.
Video na machapisho kadhaa ya mtandaoni yanaonesha Asake akiwa na baba yake, binti yake (Zeenat), na baby mama wake, wakiunda picha ya umoja wa familia.
Kabla ya maridhiano hayo, Machi, 2025, kulikuwa na ripoti na mijadala mtandaoni kuhusu uhusiano wa Asake na baba yake baada ya kusambaa kwa video za baba yake akiomba msaada na kudai kupuuzwa na kijana wake.
Chanzo; Mwananchi Scoop