Rapa wa Marekani, Wiz Khalifa ametangaza rasmi kuacha kunywa pombe, huku akisema hawezi kuruhusu tena kiasi chochote cha pombe kuingia mwilini mwake.
"Nilishaacha kunywa pombe kabla na sasa naweza kusema tena, kwamba hakuna pombe yoyote itakayoweza kuingia mwilini mwangu kamwe," amesema
Wiz Khalifa anadai hata alipojaribu kunywa pombe mara moja tu kwa wiki bado mwili wake ulishindwa kuhimili.
"Nimepunguza hadi kinywa mara moja kwa wiki lakini mwili wangu hauwezi hata kushughulikia hicho tena. Hangovers zinahisi kama milango ya mbinguni inafunguka na hiyo haifai kwa starehe ya muda mfupi," amesema Khalifa.
Aidha, rapa huyo aliongeza kuwa unywaji wa pombe hauwezi kuleta furaha ya kweli zaidi ya kufanya mambo yasiyoeleweka.
“Zaidi ya yote, si starehe hata kidogo. Yote ninayofanya ni kusema maneno yasiyo na maana na kulala kwenye kochi nikiwa nimevaa nguo zote. Niko sawa imatosha," amesema Khalifa.
Chanzo; Mwananchi Scoop