Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Eminem Msanii Mwenye Pesa Asiyejionesha Mtandaoni

Nyumba, magari, mavazi, mahusiano na vinginevyo ni miongoni mwa vitu ambavyo wasanii na watu maarufu duniani hupenda kuonyesha mitandaoni kama sehemu ya kujenga taswira ya maisha yao.

Mitandao ya kijamii imegeuka kuwa majukwaa ya kuonyesha utajiri, mafanikio na anasa, huku kila chapisho likiwa na ujumbe kwa mashabiki kuhusu maisha wanayoishi mastaa.

Hata hivyo, siyo kila msanii hufanya hivyo, wapo wanaoamini umaarufu haupimwi kwa vitu unavyoonyesha, bali kwa kazi unayoifanya na mizizi unayoitambua. Miongoni mwa majina yanayokwenda kinyume na mtazamo huo ni rapa maarufu wa Marekani, Marshall Bruce Mathers maarufu Eminem (53), aliyeanza fani hiyo miaka ya 1988.

Licha ya kuwa miongoni mwa wasanii wanaouza zaidi katika historia ya muziki wa dunia na kujikusanyia utajiri unaokadiriwa kufikia dola milioni 250, Eminem ameendelea kuishi maisha ya kawaida.

Tofauti na mastaa wengi wa hip hop wanaopenda kuonyesha majumba makubwa na maisha ya kifahari mitandaoni, The Real Slim Shady amebaki jijini Detroit, mji uliopo Michigan, Marekani, mahali alipoanzia safari ya muziki.

Eminem ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 250 milioni (zaidi ya Sh550 bilioni) na anatambuliwa kama mmoja wa wasanii wanaouza zaidi katika historia ya muziki akiwa ameuza zaidi ya rekodi milioni 220 duniani, na nakala milioni 228.5 zilizothibitishwa nchini Marekani. Rapa huyo mshindi wa Tuzo ya Oscar amenunua nyumba tatu hadi sasa akichagua mtindo wa maisha wa kawaida kuliko anasa za kupindukia kama ilivyo kwa mastaa wengine.

Eminem bado anaishi Detroit na hajununua nyumba nyingine kwa zaidi ya miaka 20 sasa ikiwa ni ishara ya uhusiano wake wa dhati na mji anaouita nyumbani. Kwa sauti kali na mashambulizi ya maneno, Eminem alivunja mipaka ya muziki wa hip-hop uliokuwa ukitawaliwa na wasanii weusi akageuza maumivu kuwa mashairi yenye nguvu.

 

 

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: