Rapa Drake amefanikiwa kutengeneza Trilioni 2.2 kwa tour zake, rekodi ambayo inampeleka msanii huyo kuwa rapa namba moja kwenye historia ya marapa waliotengeneza pesa nyingi kupitia tour na kumshusha Travis Scot, ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo, 2024, ambayo alitengeneza dola milioni 29.2.
Kwa mujibu wa Touring Data kupitia mtandao wa X, mapato yake ya ziara zake kwenye maisha ya rap dola 779 milioni sawa na trilioni 2.2 za Tanzania, ambayo inatokana tiketi milioni 6.2 alizouza katika matasha yake 513, bila kujumuisha ziara ya Some Sex Song 4 U.
Chanzo: Tanzania Journal