Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Zahir Zorro Atoa Ukweli Uvumii Unazagaa Mitandaoni

Mwanamuziki mkongwe wa Dansi, Zahir Zorro, ametoa ufafanuzi kufuatia ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya Facebook ulioibua taharuki kwa mashabiki na wadau wa muziki.

Katika ujumbe uliosambaa kwa kasi mitandaoni, Zorro aliandika: "Nahitaji mashine saba za kuzima moto nizikwe nazo kwanini? Nafahamu niendako."

Pia akaandika: "Chilling Kisota. Marafiki wamenitakia Toba leo. Nisiende na mashine 7 za kuzima moto!"

Kauli hizo zimewafanya wengi kudhani huenda msanii huyo anapitia changamoto za kiafya au maisha.

Mwananchi imezungumza na Zahir Zorro ambapo amesema ujumbe kama huo ni sehemu ya ubunifu wake wa maudhui, akisisitiza kuwa mashabiki hawapaswi kuwa na taharuki.

"Ujumbe ninaoposti kwenye akaunti yangu ya Facebook ni vibonzo. Watu waache taharuki, akaunti yangu ni biashara, mimi ni creator (muundaji), vitu vyote ninavyoweka ninavitengeneza nalipwa na Facebook," amesema Zorro.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: