Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

P Diddy Kesi 70 Zinamuamdama Licha ya Kifungo

Licha msanii na mfanyabiashara P Diddy kuhukumiwa zaidi ya miaka minne jela, bado anaripotiwa kuwa na kesi za madai za unyanyasaji wa kijinsia karibu 70 zinazomsubiri. 

Oktoba 3, Diddy alihukumiwa kifungo cha miezi 50 jela kwa mashtaka ya ukahaba yanayohusiana na kesi yake ya usafirishaji binadamu kwa ajili ya shughuli za kingono nk. Wanasheria nguli wa Bad Boy bado wanakazi kubya ya kupambana na kesi kadhaa zinazomshtaki Diddy kwa unyanyasaji wa kijinsia, zilizoanza tangu 1991, kwa mujibu wa jarida la USA Today, kesi zaidi ya 70 zimewasilishwa na ziko hai hadi sasa.

Kesi nyingi zinafanana, ambapo wengi wa wanaodaiwa kuumizwa wanasema walipewa mwaliko kwenye sherehe iliyoandaliwa na Diddy ambapo walipewa vinywaji vilivyochanganywa na madawa, na baadaye waliamka wakati au baada ya kunyanyaswa kijinsia na Diddy.

 Kesi nyingi zimewasilishwa na wakili wa Texas, Tony Buzbee, ambaye mwaka jana alidai kuwa na watu 125 tayari kuwasilisha malalamiko dhidi ya P Diddy. 

Ambapo amedai kesi chache zimesuluhishwa kama ya Cassie na nyingine zimefutwa kabisa. 

Pamoja na yote Wanasheria wa P Diddy wamekanusha madai yote "Bwana Diddy na timu yake ya wanasheria wana imani kamili na ukweli na uadilifu wa mchakato wa mahakama," 

Taarifa iliyotolewa na timu ya P Diddy inasema “Mahakamami ukweli utashinda, kwamba Bwana Combs hakuwahi kunyanyasa au kusafirisha mtu yeyote kwa njia ya ngono mwanaume au mwanamke, mtu mzima au mtoto." 

Ikumbukwe, Ijumaa Oktoba 3,2025, Diddy alihukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi miwili jela kwa kukiuka Sheria ya Mann Act. Zaidi, Wanasheria wake wanapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: