Mfanyabiashara maarufu Kim Kardashian ameandika historia mpya baada ya thamani ya kampuni yake ya mavazi Skims, kupanda hadi kufikia dola bilioni 5. Hatua iliyomfanya kuwa na utajiri wa Dola Bilioni 1.9 kwa mujibu wa Forbes
Inaelezwa kuwa ongezeko kubwa la makoto hayo limetokana na uwekezaji mkubwa wa kampuni hiyo ikipokea dola milioni 225, jambo lililowashangaza wafanyabiashara mbalimbali kutokana na na kasi hiyo ya ukuaji.
Kwa sasa Skims ina thamani kubwa zaidi ya chapa kongwe kama ‘Victoria’s Secret, hatua inayoonesha jinsi chapa hiyo inavyoongeza ushindani na kuwaumiza kichwa wamiliki wa kampuni wenye majina yaliyotawala kwa miaka mingi.
Kupanda kwa thamani ya Skims kumeifanya hisa anazomiliki Kim ndani ya kampuni hiyo kuwa zaidi ya dola bilioni 1, na hivyo kuinua utajiri wake wote hadi takribani dola bilioni 2.
Aidha inaelezwa kuwa utajiri huo umemuweka kwenye nafasi nzuri kwa familia yake pia kwani kwasasa ndiye mwanachama tajiri Zaidi wa familia ya Kardashian-Jenner.
Kampuni ya Skims iliyoanzishwa mwaka 2019, inajulikana kwa utengenezaji wa mavazi ya ndani yajulikanayo kama (shapewear), chupi, mavazi ya kupumzikia nyumbani (loungewear), mavazi ya kuogelea, pamoja na nguo za wanaume na wanawake wajawazito. Bidhaa zake zinapendwa na kukubalika Zaidi kutokana na vitambaa laini vinavyotumika kutengeneza nguo hizo.
Chanzo; Mwananchi Scoop