Davido amepoteza dau la Milioni 182 baada ya Nigeria kushindwa kupata ushindi dhidi ya Morocco katika nusu-fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2025.
Msanii huyo alikuwa ameweka dau la $50,000 (takriban Milioni 182) akiamini Super Eagles watashinda dhidi ya mwenyeji Morocco na kwa timu zote mbili kufunga goli.
Kabla ya mechi Davido alionyesha mkeka wake kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika “Nigeria wataingia fainali na nitazidisha dau langu kwenye slip yangu.”
Mechi ya nusu fainali Mchezo ulimalizika kwa sare ya 0-0 baada ya muda wa kawaida, na Morocco kushinda 4-2 kwa penati, na hivyo kuiondoa Nigeria kwenye mashindano.
Iwapo utabiri wa Davido ungefanikiwa, angepata zaidi ya $348,274, sawa na zaidi ya Bilioni 1.93
Chanzo; Bongo 5