Baada ya Kushinda Tuzo ya AFRIMA Msanii wa Bongo Fleva Juma Mussa Mkambala Maarufu kama Jux leo Januari 28, 2026 Jijini Dar es Salaam amesema Wanamuziki wa Tanzania wanatakiwa kushirikiana na Kuwa Wamoja kwenye kazi za Sanaa ili kuleta Tuzo mbalimbali nchini.
"Sio rahisi sana lakini sio kwamba haiwezekani,inawezekana kuleta tuzo kama tutashirikiana,mara ya kwanza kabisa tulikuwa na Msanii ambaye ana nafasi kubwa nje ambaye ni Diamond Platnumz lakini kutokana na kushirikiana tumeanza kuona vitu vinabadilika,hamna kitu kibaya unasafiri kwenda kwenye Show unajikuta peke yako wakati kuna Wasanii zaidi ya 10" Amesema Jux
Chanzo;Millard Ayo