Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

A$ap Rocky Ageuka Mwalimu wa Darasa la Nne Nyumbani Kwao

Rapa wa Marekani A$ap Rocky alirudi katika mji aliyozaliwa wa Harlem na kuingia kama mwalimu mbadala wa darasa la nne katika moja ya shule inayopatikana mjini hapo.

Rocky alishea momenti za furaha na wanafunzi akiwafundisha watoto jinsi ya kurapu, kisha akawasaidia kuandaa wimbo mpya unaoitwa "IDK", uliotokana na wimbo wake "Punk Rocky" unaopatikana katika albamu yake mpya, Dont Be Dumb.

Rocky alikuwa mwalimu mbadala katika darasa hilo ambalo huwakutanisha wanafunzi na mastaa mbalimbali ambao kushea maarifa na furaha pamoja na wanafunzi ambao pia hupata muda wa kuuliza maswali.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa A$ap Rocky na wanafunzi hao ni pamoja na kama atamuoa Rihanna?, Anaumri wa miaka mingapi?, Kabla ya kuanza kurapu alikuwa anafanya mishe gani?, na maswali mengine mengi.

A$ap alifanikiwa kushuti pia video ya wimbo wa IDK akiwa darasani na watoto hao. Hatahivyo mashabiki wengi mitandaoni wamesifia kitendo alichofanya wengi wakisema watoto hao hawatakuja kusahau momenti hiyo, na wengine wakitoa historia zao jinsi walivyotembelewa na mastaa wakubwa shuleni pindi wakiwa wadogo.

Utakumbuka pia A$ap Rocky amekuwa akijihusisha na mambo ya kijamii kwa kipindi kirefu kwani mwaka huu Januari aliwalipia kodi wakazi wa nyumba ya zamani aliyokuwa akiishi katika mji wa Harlem.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: