Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Denzel, Furaha Kwenye Ndoa Msikilize Mke

Kuelekea siku ya Wapendanao mwigizaji maarufu kutoka Marekani Denzel Washington, ameendelea kutoa ushauri kwa wanandoa, akielekeza namna ya kuishi kwa furaha katika ndoa zao.

Staa huyo wa Hollywood amesema siri ya kuishi kwenye ndoa ya furaha ni kumsikiliza mkeo kwa chochote anachosema au kuelezea.

“Ah… siri ya ndoa yenye furaha? Ni kufanya chochote mkeo anachokwambia. Ukitazama suala hili kwa uzito, unapaswa kumheshimu mke wako. Sikiliza anasema nini, maisha ya ndoa ni kama mpira wa kikapu huwezi kushinda ukiwa peke yako. Inahitaji kushirikiana, heshima, na kucheka pamoja hata wakati mambo si rahisi.

“Baada ya miaka mingi ya ndoa, nimejifunza kwamba uhusiano mzuri huanza na kusikilizana. Wakati mwingine unafanya kile mkeo anasema si kwa sababu ni lazima, bali kwa sababu anaweza kukuonyesha upendo kwa njia unayopaswa kuelewa. Fanya kazi pamoja, kucheka pamoja na kumbuka kila siku kwamba mke wako ni mshirika wako wa maisha. Hiyo ndiyo siri,”ameongezea Denzel

Denzel Washington na mke wake Pauletta Washington walifunga ndoa mwaka 1977. Yaani wamekaa pamoja kwa zaidi ya miaka 45. Huku wakifanikiwa kupata watoto wanne pamoja ambao ni John David, Katia, Olivia, na Malcolm.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: