Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) limewataka Waongoza Sherehe, Burudani na Matukio (MC) na Manju Muziki (DJ) kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya BASATA ili kujishughulisha na kazi za sanaa Kisheria, ikiwa ni kwa mujibu wa Kanuni za Mwaka 2018 na Tozo za Mwaka 2025, ambapo BASATA ndiyo msajili mkuu na mtoa vibali.
Wahusika wote wametakiwa kuwa na kibali hai ifikapo Januari 31, 2026, ambapo ada ya usajili ni Tsh. 10,000/= na ada ya kibali ni Tsh. 40,000/=, ikielezwa kuwa watakaokiuka watachukuliwa hatua za Kisheria.
Chanzo; Jamii Forums