Mwanamuziki wa R&B, R Kelly aliyewahi kutamba na ngoma kama I Believe I Can Fly, The World’s Greatest, Storm Is Over Now na nyinginezo ameleza huzuni yake kubwa akiwa gerezani, akidai karibia mwaka sasa hakuna mtu wa familia yake aliyemtembelea.
Katika maelezo yake yaliyochapishwa katika tovuti ya ‘ValidUpdates’ Kelly anasema moja ya jambo ambalo linamuumiza ni upweke. Hapo awali alikuwa msaada mkubwa kwa marafiki na ndugu kabla ya kuingia gerezani, lakini sasa anahisi uhusiano na watu hao umekwisha kwani anajiona kama yupo mwenyewe kwenye hii dunia.
Pamoja na maumivu hayo baadhi ya maofisa wanasema kwasasa msanii huyo amekuwa karibu zaidi na Mungu, akiomba kama siku moja marafiki pamoja na ndugu watakwenda kumtembelea tena kama ambavyo walikuwa wakifanya pindi yupo uraiani.
Utakumbuka binti wa Kelly aitwaye Joanne ‘Buku Abi’ kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni aliwahi kuweka wazi sababu ya kutomtembelea baba yake gerezani. Akidai uhusiano wake na baba yake ulishavunjika muda mrefu kutokana na makosa makubwa aliyohukumiwa.
Amesema licha ya kumpenda sana baba yake alipokuwa mdogo, maisha yalimgeuka baada ya kushuhudia madhara ya vitendo hivyo ndani ya familia.
Chanzo; Mwananchi Scoop