Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waje Adai Kutolipwa na P Square Wimbo wa “Do Me”

Mwimbaji mahiri wa Nigeria, Waje, amefichua kuwa hakuwahi kulipwa wala kutambuliwa rasmi licha ya kutoa sauti ya chorus katika moja ya vibao vikubwa vya P-Square, “Do Me”, kilichotoka mwaka 2007.

Akizungumza kupitia The Honest Bunch Podcast, Waje alisema kuwa sauti ya mwanamke inayosikika kwenye “Do Me, I do you…” ni yake, lakini hakupata hata senti moja kutokana na mafanikio ya wimbo huo. Ameeleza kuwa wakati huo alikuwa msanii chipukizi, hakuwa na uelewa wa masuala ya mikataba ya muziki, na alifanya kazi hiyo bila makubaliano yoyote ya malipo au mikopo ya kazi (credits).

Waje aliongeza kuwa licha ya wimbo huo kuhit sana Nigeria na Afrika kwa ujumla, hakuwahi kutajwa kwenye maandishi ya wimbo huo, jambo ambalo lilimfanya wakati mwingine kukosa kuaminika alipowaambia watu kuwa sauti hiyo ni yake. Alikumbuka tukio alipokuwa Onitsha sokoni na kusikia wimbo huo ukichezwa, lakini watu hawakuamini alipojitambulisha kama msanii aliyeimba kipande hicho.

Kwa upande wa P-Square, mpaka sasa hakuna taarifa rasmi wala majibu yao kuhusu madai hayo.

Wimbo “Do Me” uliwahi kuwa moja ya ngoma zilizotikisa bara la Afrika mwishoni mwa miaka ya 2000, na mafanikio yake yanakadiriwa kuwa makubwa sana katika kujenga jina la kundi hilo la mapacha.

Kwa sasa, kauli ya Waje imeibua mjadala mpana kuhusu changamoto za wasanii chipukizi, hasa pale wanapotoa mchango mkubwa bila mikataba, malipo, au utambuzi muhimu ndani ya tasnia ya muziki.

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: