Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Asap Rocky “Mama Aliniambia Rihanna Ndio Mwanamke Sahihi”

Rapa maarufu kutoka Marekani, A$AP Rocky, ameweka wazi kuwa mama yake mzazi ndiye aliyekuwa na mchango mkubwa katika uamuzi wake wa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na nyota wa muziki kimataifa, Rihanna.

Akizungumza kwenye mahojiano ya ‘NYT Popcast’ Rocky amesema mama yake alikuwa akimshauri mara kwa mara aache mahusiano mengine na amchague Rihanna, kipindi ambacho yeye na Riri walikuwa ni marafiki wa karibu tu.

Kwa mujibu wa rapa huyo, mama yake alikuwa akimuambia wazi kuwa Rihanna alikuwa mwanamke sahihi kwake, licha ya yeye mwenyewe kutokuwa na uhakika wakati huo.

“Mama yangu alikuwa akiniambia, ‘Ninajua una msichana wako, sitaki kuwataja majina, lakini nataka uwe na RiRi.

“Nilikuwa namwambia, ‘Mama, kwa nini unaendelea kusema hivyo? Hata hanipendi mimi hivyo,’” alisema Rocky huku akikiri kuwa alichukulia ushauri huo kama mzaha mwanzoni.

Hata hivyo, A$AP Rocky amesema mama yake alikuwa anamwona Rihanna kama mwanamke wa kipekee, mwenye uhalisia, misimamo na maadili ambayo yangemfaa kama mwenzi wa maisha, si kwa umaarufu wake bali kwa utu wake.

“Mama yangu alimwona Rihanna kama mtu wa kweli, mtu halisi, na mtu sahihi kwenye maisha yangu. Kweli nimegundua Mama huwa wanajua yaliyo bora,” alieleza.

Mahusiano ya Rihanna na A$AP Rocky yalianza rasmi mwaka 2020, baada ya wawili hao kuwa marafiki wa karibu kwa takribani miaka minane tangu walipoanza urafiki wao 2012.

Wawili hao walithibitisha rasmi mahusiano yao kwa umma mwaka huo huo 2020, huku wakionekana kwenye matukio makubwa ya fashion pamoja na hafla kubwa za kimataifa.

Mpaka kufikia sasa, Rihanna na A$AP Rocky wamejaaliwa kupata watoto watatu. Mtoto wao wa kwanza, RZA Athelston Mayers, alizaliwa Mei 2022, huku mtoto wa pili, Riot Rose Mayers, akizaliwa Agosti 2023 na watatu akiwa Rocki ambaye ana miezi mine tu.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: