Malkia wa kiwanda cha Bongoflava, Yammi amekanusha stori za kugombana na boss wake wa zamani ambaye ni CEO wa African Princess, Nandy. Yammi ameyasema hayo ikiwa ni baada ya kukutana na waandishi wa habari siku ya Jumatano Juni 4 kutangaza ujio mpya wa ngoma mpya.
Yammi ambaye kwa sasa yuko chini ya menejimenti mpya amesisitiza kumalizana kwa amani na Nandy huku akimshukuru boss wake huyo wa zamani kumfikisha hapo alipo kwa sasa kimuziki.