Ikiwa wameadhimisha mwaka mmoja wa ndoa hivi karibuni, Jux ameendelea kutoa nyimbo ambazo kwa asilimia kubwa jumbe zake amezielekeza kwa mkewe Priscilla ambaye naye ameonyesha ushirikiano.
Tayari Jux ametoa nyimbo tano maalum kwa Priscilla huku bibie akitokea katika video zake zote. Je, nyimbo hizo ni zipi?, zinazungumzia nini hasa na zilitoka wakati gani?.
1. Ololufe Mi (2024) Picha Linaanza
Katika video ya wimbo huu, Jux na Diamond Platnumz wamecheza kama watoto wa Mfalme mwenye nguvu kubwa kiutawala. Baba yao huyo amewachagulia wanawake wa kuoa ila tayari kila mmoja ana chaguo lake.
Jux amempenda Priscy kutokea Nigeria ambaye alijuana naye kupitia mitandaoni, huku Diamond akiangukia kwa mtumishi anayefanya kazi katika Ufalme wao kitu ambacho ni kinyume na matakwa ya baba yao.
Wanajadili ikiwa ni sawa kuacha urithi wa Ufalme ili kufuata kule walipopenda, Diamond anamshauri Jux kuusikiliza moyo wake ingawa yeye mwenyewe mwanzoni alipanga kuheshimu chaguo la mfalme.
Mwisho wa siku wote wanafuata nyoyo zao na sio matakwa ya baba yao, kufikia hapo mfalme anakuwa hana jinsi zaidi ya kubariki uamuzi wa watoto wake na hivyo ndoa mbili zinafungwa ambapo Jux anamuoa Priscilla.
2. Si Mimi (2025) - Uchumba
Jux alitoa wimbo huu muda mfupi baada ya kumchumbia Priscilla, humu anasema yote anayomfanyia mkewe si yeye ni akili yake, moyo wake, mawazo, na labda ni roho yake.
Video yake inaonyesha tukio la Jux kuvishwa pete Priscilla, tukio ambalo lilihudhuriwa na baadhi ya watu mashuhuri kutoka Tanzania pamoja na Nigeria.
Chanzo; Mwananchi Scoop