Ikiwa ni masaa kadhaa tangu vita ya maneno itokee baina ya mafahari wawili wa Hip Hop nchini, Nay wa Mitego na Billnas na kufanya mashabiki wengi wahoji nini kinaendelea bila kupata majibu, Billnas ameeleza chanzo cha ugomvi huo ambapo amemrushia lawama Nay wa Mitego kwa kutaka kumgeuza mhanga.
Billnas amezungumza hayo wakati wa mahojiano na East Africa Radio ambapo ameeleza kusikitishwa na kinachoendelea.