Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Zawadi Zaongezwa Kombe la Shirikisho Mshindi wa 1 Bilioni 10

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limetangaza ongezeko kubwa la zawadi za fedha kwa mashindano ya CAF Confederation Cup msimu wa 2025/2026, hatua inayolenga kuimarisha klabu za Afrika kifedha na kiushindani.

Kwa mujibu wa mgawanyo huo mpya wa fedha:

🏆 Mabingwa watatunukiwa dola milioni 4 za Marekani (Sh10.4 bilioni).

🥈 Washindi wa pili watajinyakulia dola milioni 1 (Sh2.6 bilioni).

🔹 Timu zitakazofika hatua ya nusu fainali zitapata dola 750,000 (Sh1.95 bilioni) kila moja.

🔹 Timu za robo fainali zitazawadiwa dola 550,000 (Sh1.43 bilioni) kila moja.

🔹 Timu zitakazomaliza katika nafasi ya tatu na nne kwenye hatua ya makundi zitapokea dola 400,000 (Sh1.04 bilioni). kila moja.

Ongezeko hili la fedha linatajwa kuwa kichocheo muhimu kwa maendeleo ya soka la vilabu barani Afrika, likitoa motisha zaidi kwa timu kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Hatua hii pia inatarajiwa kuongeza ushindani, uwekezaji, na ubora wa soka katika ngazi ya klabu kote barani. 

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: