FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa mchezo wao dhidi ya Al Masry hautakuwa mwepesi kulingana na wapinzani wao walivyo lakini malengo makubwa kwao ni kupata mabao ugenini kwa kuwa itakuwa ni faida kwao.
Kikosi cha Simba kipo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry amba oni hatua yar obo fainali unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025. Ikumbukwe kwamba Machi 28 kikosi cha Simba kilikwea pipa kutoka Tanzania mpaka Cairo kisha wakaelekea kuweka kambi katika mji wa Ismailia ambapo waliweka kambi kwa maandalizi ya mchezo huo.
“Tunaendelea na maandalizi ambapo wachezaji wanajitahidi kuendana na mazingira ya hali ya hewa ambayo yapo kwa sasa na tupo tayari kwa kuwa wachezaji wapo tayari kuelekea mchezo wetu na hakuna presha ambayo ipo kuelekea kwenye mchezo wetu. “Ukiangalia rekodi tumekuwa na matokeo kwenye mechi za kimataifa kwenye mechi ambazo tulicheza ugenini hivyo hilo halitupi presha kuelekea kwenye mchezo wetu. Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zina muungano mzuri. “Ukitazama namna ilivyo imara kwenye ulinzi, ushambuliaji inakuja na mitindo tofautitifauti kwenye mechi ambazo wanacheza lakini kwa yote hayo tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu.
Mechi haitakuwa nyepesi na kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tunapata mabao kwenye mchezo wetu.” Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.