Mbunge wa Korogwe Vijiji, Timotheo Mzava ameonyesha hofu kuhusu uhamasishaji wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 akitaka Serikali na wadau kuingilia kati.
Mzava ametoa kauli hiyo alipokuwa akichangia kwenye mjadala wa hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa Novemba 14, 2025 wakati akizindua bunge la 13.
Amesema bado Tanzania haijawekeza vya kutosha kwenye sekta ya michezo jambo linalotia mashaka kwenye mashindano ya mwakani.
Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu wenyeji wa fainali za AFCON 2027 nyingine zikiwa ni Uganda na Kenya na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hizo tatu kuandaa mashindano hayo.
Mzava pia ameomba hamasa ya mashindano hayo iendane na mkazo kwenye miundombinu katika vituo vya utalii ili watalii wakija wafurahie lakini kuwepo na mfumo wa kudhibiti Vyuo vya utalii ili wanaotoka kwenye humo wawe na uwezo wa kuleta tija kwenye sekta hiyo.
Fainali za AFCON 2027 zimepangwa kufanyika kuanzia Juni hadi Julai 2027 katika tarehe ambazo bado hazijawekwa wazi.
Chanzo; Mwananchi