Jiji la Riyadh linatarajia kuwa mwenyeji wa maonyesho ya kipekee ya paka yatakayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano na Maonyesho wa Riyadh kuanzia Novemba 25 hadi 26.
Zaidi ya paka 100 kutoka Saudi Arabia na mataifa mengine watashiriki katika tukio hilo la kipekee.
Mashindano hayo yatakuwa na vipengele mbalimbali ikiwemo mashindano ya usafi na mpangilio wa manyoya , pamoja na maonyesho ya spishi tofauti za paka. Lengo kuu ni kusherehekea urembo wa paka, utamaduni na urafiki wao na binadamu.
Chanzo: Dw