Shirikisho la Mpira wa Miguu Ureno (PFF), limetoa taarifa ya kutokubaliana na adhabu aliyopewa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa hilo, Cristiano Ronaldo, kutokana na tabia yake ya ukali wakati Ureno ikifungwa 2-0 dhidi ya Ireland, Novemba 13, 2025.
PFF imepanga kuwasilisha malalamiko kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) kwa lengo la kuomba Ronaldo apunguziwe muda wa adhabu ya kusimamishwa kucheza mechi zinazoratibiwa na shirikisho hilo.
Hata hivyo, jarida la Record linadai kuwa Rais wa PFF, Pedro Proenca, anajiandaa kuwasilisha malalamiko FIFA akitumaini kuepuka adhabu ya zaidi ya mechi moja kwa Ronaldo.
Ripoti hiyo inadai kuwa Ureno itajenga hoja yake kupitia malalamiko hayo kwa mambo matatu.
Chanzo; Mwananspoti