Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Msajili Apewa Siku 12 Kumaliza Utata Simba

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemtaka Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Abel Ngilangwa kuipa Simba majibu ya kinachoendelea kuhusu mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Makonda amesema kuwa msajili anatakiwa kabla ya mwezi huu kumalizika, awe ametoa majibu kwa Wanasimba.

“Msajili wa michezo nilitaka mkamilishe taratibu za Simba. Na nilitaka niwahakikishie kwamba katika kipindi ambacho sheria na kanuni zitafuatwa sana ni hiki cha uongozi wangu.

“Kamilisha na ikiwezekana kabla ya mwezi huu uwape majibu Wanasimba. Tunachotaka sisi tuone timu hizi zikifanya vizuri. Kabla ya mwezi huu, jambo hili liwe limekamilika,” amesema Makonda.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: