Nahodha wa Tottenham Hotspurs Son Heung-min ametangaza kuachana na klabu hiyo aliyoitumikia kwa misimu 10.
Son mwenye miaka 33 bado ana mkataba na Tottenham mpaka 2026, ambao hata hivyo huenda ukavunjwa mara baada ya makubaliano kufikiwa na timu ya Los Engeles FC inayoshiriki Major Soccer League ya nchini Marekani.
“Nilijiunga na klabu hii nikiwa kijana mdogo tu asiejua kuongea kiingereza na sasa naondoka nikiwa mtu mzima, najivunia sana kwa hatua hii”, amesema Son.
Son aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Asia kushinda kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora katika msimu wa 2021-22 ambapo pia anashikilia rekodi ya mchezaji wa Spurs mwenye kutoa assist nyingi, akiwa amechangia 101.