Mashabiki wa ES Tunis wametuma ujumbe i kwa wachezaji wao kabla ya pambano muhimu la Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Petro de Luanda ya Angola.
Mashabiki wa ES Tunis ambao wana nguvu ndani ya klabu hiyo ya jijini Tunis, Tunisia wametuma ujumbe huo kwa njia ya ‘bango’ maalum ambalo limechapishwa kwa maneno yanayosomeka “Kupigana uwanjani ni amri.” 🔥
Ujumbe huo unaashiria wazi kuwa hakuna nafasi ya kuhesabu au kutoa visingizio, huku mashabiki hao wakisisitiza umuhimu wa mechi ya Jumamosi ambayo itaamua hatima ya klabu hiyo hiyo kutinga robo fainali au kutolewa.
Hadi sasa, ES Tunis na Petro de Luanda zote zina pointi 6 baada ya mechi 5, hali ambayo inaifanya mechi hiyo itakayopigwa jijini Tunis, kuwa ya ushindani na yenye uamuzi wa mwisho.
Mshindi wa mechi hiyo ataungana na Stade Malien ya Mali, huku atakayepoteza akiungan na Simba ya Tanzania ambayo imeshatolewa kwenye michuano hiyo kupitia Kundi D.
Chanzo; Mwanaspoti