Bondia Anthony Joshua amejeruhiwa, huku watu wengine wawili wakifariki dunia, katika ajali ya gari iliyotokea Nigeria.
Polisi wa eneo hilo wanaeleza kuwa Joshua amepelekwa hospitalini baada ya kupata majeraha madogo na yupo salama.
Ajali hiyo imetokea leo siku ya Jumatatu kwenye barabara kuu ya Ogun–Lagos.
Bondia huyo wa uzani wa juu mwenye umri wa miaka 36 ana asili ya kifamilia kutoka Sagamu, mji uliopo katika Jimbo la Ogun, Nigeria.
Chanzo; Bongo 5