Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Folz Afichua Yaliyomchosha Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga, Romain Folz amedai kwamba maisha ndani ya timu hiyo yalikuwa magumu kwake na benchi lake la ufundi jambo lililochangia kutimuliwa kwake , Oktoba 18, 2025.

Akizungumza na Jarida la KICKOff katika toleo la Januari, Folz, ambaye alishinda taji moja wakati wa kipindi chake klabuni hapo, alifichua kuwa kufukuzwa kwake hakukutokana na matokeo uwanjani, bali ni matatizo ya nje ya uwanja ambayo hakuweza tena kuyavumilia.

“Ninafanya kazi ili kushinda, hivyo kukusanya mataji huwa ni jambo zuri kila wakati. Kufukuzwa kwangu kulikuwa ni matokeo ya upuuzi mwingi ambao mimi na benchi langu la ufundi tulilazimika kuupitia.

“Maandalizi yetu yalivurugwa sana ndani ya klabu, na nilikuwa napinga hali hiyo kwa nguvu zote. Bila hayo, nisingepoteza hata mchezo mmoja naweza kukuhakikishia hilo.

“Hivi sivyo ninavyofanya kazi, na sivumilii upuuzi. Nilifukuzwa baada ya kipigo changu cha kwanza na cha pekee, nikiwa nimefungwa bao moja tu kwa jumla. Kipigo hicho hakikuhusiana nami wala benchi langu la ufundi,” amesema Folz.

Folz amesema kuwa yeye na benchi lake la ufundi walitimiza vyema wajibu wao.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: